MASKINI
NA KUKU WA DHAHABU
Palitokea ugeni wa watu kutoka nchi ya mbali
kutembelea kijiji cha Sisi Tupo tu, lengo la ujio wao ulikuwa ni kutembelea
kuona umaskini wa kijiji hiki. Ziara haikuwa ya muda mrefu kipindi wanaondoka
walimwachia mmoja wa wana kijiji kuku mmoja. Na ajabu usiku ule mwanakijiji
alipoamka alikuta kuku yule kabadilika rangi akiwa na mbawa za dhahabu, na cha
ajabu zaidi chini akakuta mayai ya dhahabu. Furaha ikamjaa kutamani asubuhi
ifike ili aende kijiji cha mbali kuuza, ilipofika asubuhi alienda kuuza yale
mayai kijiji cha mbali na akarudi kafanya manunuzi mengi ikiwepo chakula,
makochi na mahitaji mbalimbali. Kadri siku zilivyokuwa zinaenda kuku alikuwa
akitaga mayai mengi na yote ya dhahabu, maskini huyu alijikuta anaendelea
kutajirika zaidi na zaidi. Wakati huu aliweza kununua gari na hata kujenga
nyumba kwa muda mfupi,
Baada ya mwezi mmoja kupita kuku akawa anakaa baada
ya muda kisha anataga mayai, na huu msimu mwanakijiji huyu alikuwa akihutaji
kununua ndege kubwa na aliona kuku akichelewa kutaga mayai ili akauze apate
fedha za kununua, uamuzi aliochukua ni kumchukua kuku na kumchija, akidhani
kupata mayai ndani, cha kusikitisha hakuona chochote na kuku alikuwa amekwisha
kufa.
Kwa kuwa gharama za maisha zilimwihitaji kula,
alijikuta akianza kuuza mali zake, siku akiwa katika njia alionana na moja ya
wateja wake wa mayai, na mteja huyu alijawa na furaha kubwa mno usoni
alipomwona mwanakijiji huyu, na baada ya salamu akatanguliza neno nashukuru
sana, yale mayai ulonipa nilitotolesha na kupata kuku wengi zaidi, na hawa kuku
walitoa mayai ya dhahabu na ninao kuku wa mbawa za dhahabu wengi zaidi. Wakiwa
katika kuongea ujio wa wale wageni ukarudi siku hiyo na kumkuta aliyepewa kuku
karudi kawa maskini na wengine waliouziwa mayai ni matajiri. Maskini
mwanakijiji hakujua ndani ya yai kulikuwa na kuku wengi, yeye akauza mayai
yenye kuku ndani.
Funzo ni muhimu kutumia fedha kuzalisha zaidi kuliko
kuishia kuitumia pasipo kuizalisha zaidi.
Na Raymond Mgeni....0676559211/0766461571