Alhamisi, 23 Machi 2017


MASKINI NA KUKU WA DHAHABU

Palitokea ugeni wa watu kutoka nchi ya mbali kutembelea kijiji cha Sisi Tupo tu, lengo la ujio wao ulikuwa ni kutembelea kuona umaskini wa kijiji hiki. Ziara haikuwa ya muda mrefu kipindi wanaondoka walimwachia mmoja wa wana kijiji kuku mmoja. Na ajabu usiku ule mwanakijiji alipoamka alikuta kuku yule kabadilika rangi akiwa na mbawa za dhahabu, na cha ajabu zaidi chini akakuta mayai ya dhahabu. Furaha ikamjaa kutamani asubuhi ifike ili aende kijiji cha mbali kuuza, ilipofika asubuhi alienda kuuza yale mayai kijiji cha mbali na akarudi kafanya manunuzi mengi ikiwepo chakula, makochi na mahitaji mbalimbali. Kadri siku zilivyokuwa zinaenda kuku alikuwa akitaga mayai mengi na yote ya dhahabu, maskini huyu alijikuta anaendelea kutajirika zaidi na zaidi. Wakati huu aliweza kununua gari na hata kujenga nyumba kwa muda mfupi,

Baada ya mwezi mmoja kupita kuku akawa anakaa baada ya muda kisha anataga mayai, na huu msimu mwanakijiji huyu alikuwa akihutaji kununua ndege kubwa na aliona kuku akichelewa kutaga mayai ili akauze apate fedha za kununua, uamuzi aliochukua ni kumchukua kuku na kumchija, akidhani kupata mayai ndani, cha kusikitisha hakuona chochote na kuku alikuwa amekwisha kufa.

Kwa kuwa gharama za maisha zilimwihitaji kula, alijikuta akianza kuuza mali zake, siku akiwa katika njia alionana na moja ya wateja wake wa mayai, na mteja huyu alijawa na furaha kubwa mno usoni alipomwona mwanakijiji huyu, na baada ya salamu akatanguliza neno nashukuru sana, yale mayai ulonipa nilitotolesha na kupata kuku wengi zaidi, na hawa kuku walitoa mayai ya dhahabu na ninao kuku wa mbawa za dhahabu wengi zaidi. Wakiwa katika kuongea ujio wa wale wageni ukarudi siku hiyo na kumkuta aliyepewa kuku karudi kawa maskini na wengine waliouziwa mayai ni matajiri. Maskini mwanakijiji hakujua ndani ya yai kulikuwa na kuku wengi, yeye akauza mayai yenye kuku ndani.

Funzo ni muhimu kutumia fedha kuzalisha zaidi kuliko kuishia kuitumia pasipo kuizalisha zaidi.

 Na Raymond Mgeni....0676559211/0766461571

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni